RC KIHONGOSI AKABIDHI MAGARI KWA WAKUU WA WILAYA 3 SIMIYU. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 9 July 2024

RC KIHONGOSI AKABIDHI MAGARI KWA WAKUU WA WILAYA 3 SIMIYU.

*AWATAKA KUYATUNZA, KUYATUMIA KUWAFIKIA WANANCHI ILI KUTATUA KERO ZAO.*


Bariadi-Nyaumata,


Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Kenan Laban Kihongosi Leo 9 Julai 2024 amekabidhi Magari kwa Wakuu wa Wilaya watatu Mkoani humo.


Wakuu wa Wilaya waliokabidhiwa magari hayo aina ya Prado TXL ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe.Aswege Kaminyoge,Mkuu wa Wilaya ya Meatu Mhe.Faudhia Ngatumbura pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mhe.Anna Joram Gidarya.


Akizungumza mara baada ya kukabidhi Magari hayo Mhe.Kihongosi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Magari wakuu hao wa Wilaya ambapo ameeleza kuwa Magari hayo yatasaidia Viongozi hao kuwafikia Wananchi kwa urahisi kusikiliza na kutatua kero zao.


Amewataka Wakuu wa Wilaya waliopatiwa Magari hayo kuyatunza pamoja na kuyatumia kwa malengo mahsusi ya kuwafikia Wananchi kwa urahisi Ili kutatua changamoto zao.


Kwa upande wao wakuu wa Wilaya waliokabidhiwa magari hayo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia Magari hayo ambapo wameahidi kuyatumia Magari hayo kwa malengo yaliyokusudiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso