KUPITIA WATUMISHI WA UMMA SERIKALI INAFUATILIA MAHITAJI YA WANANCHI - MAJALIWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 9 July 2024

KUPITIA WATUMISHI WA UMMA SERIKALI INAFUATILIA MAHITAJI YA WANANCHI - MAJALIWAWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa amehutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa MwembeTogwa kwenye Manispaa ya Iringa, Julai 8, 2024.


Akizungumza katika mkutano huo Mheshimiwa Majaliwa amesema uimara wa Serikali yoyote ni pamoja na uwepo wa watumishi wa umma na kupitia wao, Serikali inafuatilia mahitaji ya wananchi kwenye maeneo yote.


“Serikali yenu chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kufuatilia mahitaji ya wananchi. Katika kufuatilia, tumezihusisha Halmashauri za Wilaya kote nchini kuhakikisha kuwa zinawafikia kwenye vijiji mlipo, mnaeleza matatizo mliyonayo na wao wanaratibu kwa kuanza utatuzi wa kero zinazowagusa kwenye maeneo yenu.”

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso