MADETE AVULIWA UONGOZI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 13 June 2024

MADETE AVULIWA UONGOZI UVCCM WILAYA YA SHINYANGA MJINI
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga CCM imemuachisha nafasi ya uongozi aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama hicho wilaya ya Shinyanga Mjini Ndg. Jonathan Agustino Madete kwa sababu ya utovu wa nidhamu.Maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia kikao kilichoketi leo Juni 13, 2024 katika jingo la ofisi ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga zilizopo manispaa ya Shinyanga.

Akisoma maamuzi yaliyofikiwa na kikao hicho wakati akizungumza na vyombo vya habari Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga CCM Ndg. Rachard Raphael Masele amesema kikao cha halmahsauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga Mjini chini ya mwenyekiti wake Ndg. Mabala Mlolwa kimemuachisha nafasi ya uongozi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wilaya ya Shinyanga Mjini na kuazimia kutofumbia macho wala kumvumilia yeyote atakayevunja kanuni na katiba ya chama hicho.

“Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM, Mkoa wa Shinyanga chini ya Mwenyekitiwake Ndg. Mabala Mlolwa kilichoketi mnamo 13.06.2024 pamoja na mambo mengine kimemuachisha nafasi ya uongozi Ndg. Jonathan Agustino Madete aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini kwa sababu za utovu wa nidhamu”, amesema Richard Masele.

“Vile vile halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Shinyanga kamwe haitamfumbia macho wala kumvumilia mtu yeyote kiongozi au mwananchama atakayevunja kanuni, taratibu na katiba ya chama chetu, hatua za kinidhamu zitachukuliwa mala moja, hii ni pamoja na kulinda heshima ya chama chetu na jumuiya zake”, ameongeze Richard Masele.

Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga CCM Ndg. Rachard Raphael Masele akizungumza na vyombo vya habari.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini Ndg. Jonathan Agustino Madete.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso