SASA ARUSHA NI SHWARI, NIMEKULA KIAPO NA WADUDU KULINDA AMANI YA MKOA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 1 May 2024

SASA ARUSHA NI SHWARI, NIMEKULA KIAPO NA WADUDU KULINDA AMANI YA MKOA



Mkuu wa mkoa wa Arusha ,Paul Makonda akitoa salama zake katika sherehe za meimosi amesema kuwa, kuanzia leo Arusha ni mkoa shwari na salama kwa watalii na kila mtanzania na watahakikisha kila mtu anarejea nyumbani au nchini kwake akiwa salama .

Amesema kuwa ,amekula kiapo jana na wadudu kuhakikisha wanalinda amani ya mkoa wa Arusha na kuhakikisha hakuna mdudu anayechafua amani ya Arusha.

“Leo tumesherehekea meimosi bila kujali kabila wala dini na tutahakikisha tunakuwa bega kwa bega na viongozi wa Taifa kuhakikisha wanailinda amani ya nchi.”amesema Makonda.

“Hata mwezi sijamaliza ila kazi zinaenda vizuri kutokana na ushirikiano mkubwa niliopewa na Mongela ambaye ni kaka yangu na ukiona mambo yanaenda vizuri mjue kuna mikoba niliyoachiwa.”amesema

Amesema kuwa kuwepo kwa meimosi mkoani Arusha ni fursa kwa mkoa wa Arusha

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso