RC MACHA AMEAHIDI UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 15 May 2024

RC MACHA AMEAHIDI UHURU WA VYOMBO VYA HABARI MKOANI SHINYANGA




MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amewahidi Waandishi wa habari mkoani humo kwamba kutakuwepo na Uhuru wa Habari wa kutosha kwa maslahi mapana ya wananchi kupata taarifa mbalimbali.


Macha amebainisha hayo leo Mei 15,2024 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari,ambapo Klabu ya Waandishi wa Mkoa wa Shinyanga (SPC) imeadhimisha leo na Kitaifa Maadhimisho hayo yalifanyika Mei 3 mwaka huu Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.


Amesema katika Mkoa wa Shinyanga kutakuwepo na uhuru wa habari wa kutosha, na kwamba Taasisi yoyote ile ya Umma ama kiongozi atakaye Mnyima Mwandishi wa habari taarifa, awasiliane naye ili kuliona namna ya kulitatua sababu Habari ni kwa Maslahi ya wananchi.


“Mimi sijawahi kumyima Mwaandishi wa habari Taarifa katika uongozi wangu tangu nilipokuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama na sasa ni Mkuu wa Mkoa Shinyanga, kama yupo ambaye anasema niliwahi kumyima habari anyooshe Mkono,”amesema Macha.
Aidha, amesema kama kunatatizo la unyimwaji taarifa kwa Waandishi wa Habari mkoani humo analikemea, na kutoa Nasaha kwa Viongozi wa Serikali, kwamba wao ni Watumishi wa wananchi na wanawategemea kupata taarifa za Serikali kupitia Waandishi wa habari, hivyo ni vyema wasifiche taarifa bali wazitoe kwa maslahi ya umma.


Amesema kwa zile habari ambazo niza siri kwa maslahi mapana ya nchi ni vyema zisiandikwe,lakini zile ambazo zinagusa maslahi ya wananchi haina haja kuficha taarifa hizo, bali waandishi wa habari wapatiwe na kuhabarisha umma.
Amewataka pia waandishi wa habari kwamba katika uhuru huo wa kujieleza wawe na mipaka, pamoja na kufanyia utafiti taarifa zao na kubalance story ili kuondoa Migogoro na kusababisha chomba chake cha habari kuomba radhi kwa mdau na kukipunguzia uaminifu.


Uchaguzi Serikali za Mitaa.


Macha amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kwamba katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu,wasikumbatia wagombea na kuandika habari za Mtu binafsi, bali wajikite kuandika habari kwa maslahi ya umma na wasitumike pia kumchafua Mgombea mwingine.
Ujumbe kwa Wamiliki vyombo vya habari.


Ametoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari, kwamba wajali maslahi ya watumishi wao kwa kuwapatia Mikataba na Mishahara mizuri ili wafanye kazi zao kwa ufanisi na kuzingatia maadili ya taaluma yao.


Utunzaji wa Mazingira.


Amewasihi Waandishi wa habari kutumia kalamu zao kwa kupaza sauti juu ya utunzanji wa Mazingira na kucha kukata miti hovyo pamoja na kutumia Nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo yameleta madhara makubwa hapa nchini.
Ujumbe Siku ya Familia.


Akizungumzia siku ya Familia duniani,ametumia fursa hiyo kuwataka wazazi mkoani humo kuishi kwa upendo na kuacha Migogoro ya kifamilia,ambayo imekuwa ikisababisha ukatili dhidi ya watoto na hata kusabisha tatizo la watoto wa Mitaani, huku akiwaomba viongozi wa dini kusaidia pia matatizo ya ndoa.


Kazi


Amewataka waandishi wa habari mkoani humo, kuandika habari za kuhamasisha wananchi wasichangua kazi, bali wafanye kazi yoyote ambayo itawasaidia kujipatia kipato na kuendesha maisha hao.
Mwenyekiti Shinyanga Press Club.


Mwenyekiti Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru, awali akisoma taarifa ya Klabu hiyo, amesema kwa taarifa iliyotolewa na Baraza la Habari Tanzania mwaka 2022 kwamba Mkoa wa Shinyanga umeshika nafasi ya Pili kwa Waandishi wa habari kufanyiwa madhira mbalimbali ikiwamo kunyimwa taarifa kutoka Ofisi za umma na binafsi.


Aidha, ameipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kufanya marekebisho ya sheria ya vifungu 9 ya sheria ya vyombo vya habari na kuongeza uhuru wa kujieleza, na sasa Tanzania inashika nafasi ya kwanza kwa ukanda wa Afrika Mashariki, na kwa mujibu wa taarifa ya Wolrd Press Freedom kwa kushika nafasi ya 9 duniani.

“Klabu ya Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga sasa hivi tunatekeleza Mradi wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto wilayani Shinyanga, lakini kuna baadhi ya Watendaji wanawanyima taarifa waandishi wa habari, tunaomba hili Mkuu wa Mkoa ulitolee tamko ili kuwepo na uhuru wa habari hapa Shinyanga,”amesema Kakuru.


“Hivi karibuni Klabu yetu itakuwa na Mradi wa Uhuru wa kujieleza ambao utakutanisha wadau mbalimbali, na Mradi huu utawapa haki kwenu kama wadau kupaza sauti juu ya ustawi wa maendeleo ya Mkoa wetu,”ameongeza.
Kampeni ya Mazingira Shinyanga Press Club.


Ameomba wadua kushirikiana kikamilifu na Waandishi wa habari juu ya Kampeni ya utunzaji wa Mazingira ambapo Klabu hiyo hivi karibuni wanatarajia kufanya Kampeni ya utunzanji Mazingira lenye maudhui ‘Nafasi ya Vyombo vya Habari katika Mabadiliko ya Tabia nchi, kampeni ambayo itasaidia utekelezaji Mkakati wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia wa Mwaka 2024/2034.


Kauli Mbiu.


Kauli Mbiu ya Siku ya Uhuru wa vyombo vya habari duniani Mwaka huu 2024 inasema “Uandishi wa Habari na Changamoto ya Mabadiliko ya Tabia Nchi”.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso