TFF PAMOJA NA KDFA WAHITIMISHA MAFUNZO YA UKOCHA KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 24 April 2024

TFF PAMOJA NA KDFA WAHITIMISHA MAFUNZO YA UKOCHA KAHAMA


Jumla ya makocha 35 kutoka mikoa mitatu ya Geita, Tabora na Shinyanga wamehitimu kozi ya awali ya ualimu wa mpira wa miguu Grassroots (kocha) mafunzo yaliyofanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
wahitimu wa mafunzo ya ukocha (grassroot) wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongizi

 NEEMA NKUMBI HUHESO DIGITAL&HUHESO FM 

Mafunzo hayo ya siku tano yalianza rasmi April 18 na kuhitimishwa April 22, 2024 yalikuwa yakifundishwa na mkufunzi wa Kozi hiyo nchini Raymond Gweba kutoka shirikisho la soka nchini TFF.


Mgeni rasmi Felix Ntibabara ambaye ni afisa utamaduni, sanaa na michezo Manispaa ya Kahama ameshiriki zoezi la ufungaji kozi hiyo na ugawaji vyeti kwa washiriki wote amewataka washiriki kwenda kuufanyia kazi ujuzi walioupata ili kuibua vipaji kwani wilaya ya Kahama Ina vipaji vingi.


Aidha mwenyekiti wa chama Cha soka wilaya ya Kahama Salum Husein amesema kuwa timu zote ndani ya wilaya ya Kahama zinapaswa kufundishwa na makocha wenye ujuzi wa soka hivyo waliopata kozi hiyo ya Grassroots wakawe walimu wazuri na KDFA itawalinda.


Hata hivyo baadhi wahitimu wa mafunzo hayo Aisa Godson na Hamad Sule wamesema kuwa wamefurahi kupata mafunzo hayo kwani yamewasaidia kubadili mitazamo waliyokuwa nayo katika ufundishaji hivyo watayatumia vyema kuwafundisha watoto mashuleni kuleta chachu ya soka la Kahama

Makocha thelathini na moja wametoka wilaya ya Kahama, Geita wawili na Tabora wawili

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Kahama Salumu Husein akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo ya makocha


Mkufunzi wa makocha nchini Raymond Gweba kushoto akiwa na mgeni rasmi Felix Ntibabara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso