MO ATETA NA VIONGOZI SIMBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 15 April 2024

MO ATETA NA VIONGOZI SIMBA


MWEKEZAJI wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji 'Mo' amefanya kikao cha ndani na viongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Mo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na X amedokeza kuwa kikao hicho kinaenda kuwa mwarobaini wa changamoto zilizopo klabuni humo.

"Nimefanya kikao na viongozi wa Simba SC kujua changamoto zipo wapi na namna ya kuzitatua. Kikao kimeenda vizuri," ameeleza tajiri huyo kijana.

Dewji amewaomba mashabiki na wapenzi wa klabu hiyo kutokufa moyo na kuendelea kushirikiana na kushikamana katika kipindi hiki ambacho klabu hiyo haifanyi vizuri.

Simba imekuwa na matokeo mabovu hususani katika michezo yake ya hivi karibuni baada ya kufungwa michezo 2 ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) pia kuondoshwa katika michuano ya Kombe la Shirikisho la CRDB na kutoa sare dhidi ya Ihefu ugenini mkoani Singida katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso