MBUNGE WA USHETU, CHEREHANI APONGEZWA KWA ZAWADI YA MBUZI NA WANANCHI KWA KUWEZESHA MAWASILIANO YA SIMU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 7 April 2024

MBUNGE WA USHETU, CHEREHANI APONGEZWA KWA ZAWADI YA MBUZI NA WANANCHI KWA KUWEZESHA MAWASILIANO YA SIMU

Wananchi wa Kijiji cha Ngokolo katika Kata ya Bukomela halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamemuomba mbunge wa jimbo hilo la Ushetu, Emanuel cherehani kuungana nao kuhakikisha mradi wa uijenzi wa Zahanati katika kijiji hicho unakamilika.


Neema Nkumbi-Huheso FM na Huheso digital blog


Wametoa maombi hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika April 06, 2024 kijijini hapo ulioandaliwa kwa ajili ya kumpongeza kwa kuwezesha upatikanaji wa mnara wa mawasiliano ambapo kijiji cha Ngokolo kilikuwa na changamoto ya mawasiliano kwa wananchi wapatao 2300.


Akisoma risala iliyoandaliwa na wananchi katika mkutano huo kwa niaba ya wananchi, Nyanda Ngatale alisema kuwa changamoto kwa sasa iliyopo kwa sasa ni Zahanati kwa ajili ya huduma za Afya ambapo wamekuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma.

Nae kada wa chama cha mapinduzi CCM, Neema Mgeni amewaomba wananchi wa Ushetu hasa wanaume kutokuwabagua katika uongozi wanawake ili kuhakikisha wanainuka kiuchumi huku akiwaasa wanawake wa jimbo hilo kutokuogopa kuomba nafasi za uongozi na wanapopata wakapiganie haki za wanawake.


Alisema katika chama cha Ushirika KACU yupo mwanamke mmoja tu ambaye ni mjumbe hivyo ameuomba uongozi wa ushirika huo kupanua wigo wa kuongeza wanawake katika bodi yao.


Aidha kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Ushetu Emanuel Cherehani aliwahakikishia wananchi wa kijiji cha Ngokolo kuwa ukamilishaji wa Zahanati hiyo utafanyiwa kazi ili kusogeza huduma kwa wananchi.


Pia aliwataka kutumia hospitali ya halmashauri ya Ushetu kupata huduma ya vipimo vyote na tiba zinapatikana katika hospital hiyo.


Hata hivyo mbunge Emanuel Cherehani alisema kuwa mradi wa maji ziwa Victoria upo mbioni kuanza utekelezaji hivyo jimbo hilo linakwenda kuondokana na adha ya wananchi kukumbwa na changamoto ya maji.

''Jimbo la Ushetu ni kayi ya majimbo sita yaliyopo katika kwenye mkoa wa Shinyanga lakini lililobaki halikuwa na maji ya ziwa victoria ni Ushetu peke ake, tayari mheshimiwa rais Samia ametusainia bilion 46 tumepewa ushetu kwa ajili ya maji na tayari mkandarasi ameshapatikana''

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso