ICRA yajivunia kuidhinishwa na Benki Kuu - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 2 April 2024

ICRA yajivunia kuidhinishwa na Benki Kuu

WAKALA wa Ukadiriaji (ICRA), imesema inajivunia kuidhinishwa kwake kama wakala wa kwanza wa kutathmini mikopo Afrika Mashariki iliyoidhinishwa na Benki Kuu ya Tanzania.






Mkurugenzi wa ICRA, Hassan Mansur ameeleza kuwa wakala unaendelea kuimarisha uwepo wake katika eneo la Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini (MENA), huku ukipiga hatua kubwa barani Afrika.

“Utambuzi huu wa kifahari unaiweka ICRA kama wakala pekee wa kikanda wa ukadiriaji wa mikopo ulioidhinishwa na benki kuu inayotoa huduma zake. Zaidi ya hayo, ICRA imefikia hadhi tukufu ya Taasisi ya Nje ya Tathmini ya Mikopo (ECAI),” imeeleza taarifa hiyo.

Amesema wakala huo umeimarisha dhamira yake kwa Tanzania kwa kusaini Hati za Makubaliano (MOUs) na taasisi muhimu kama vile Credit Info Tanzania, Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA), Chama cha Taasisi Ndogo za Kifedha Tanzania (TAMFI), na Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB).

“Kwa kupendezwa na kuongezeka kwa wawekezaji wa kimataifa wa ICRA kutoka Uholanzi, Mauritius, Afrika Kusini, UswiSi na Ufaransa, ICRA inaangazia fursa mbalimbali za uwekezaji na ufadhili.

“ICRA yenye makao makuu yake Dubai, UAE, imekuwa ikitoa huduma za mfano za ukadiriaji wa mikopo kwa benki, taasisi za fedha na mashirika,” amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso