BOSI WA KIJIJI CHA NGURUWE AAHIDI ZAWADI YA NGURUWE ALIYENONA KWA KILA GOLI LA SIMBA SC DHIDI YA IHEFU SC - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 12 April 2024

BOSI WA KIJIJI CHA NGURUWE AAHIDI ZAWADI YA NGURUWE ALIYENONA KWA KILA GOLI LA SIMBA SC DHIDI YA IHEFU SC



Mkurugenzi wa Kampuni ya Kijiji cha Nguruwe Project kilichopo Zamahero wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma ambaye ni shabiki kindakindaki wa Timu ya Simba SC Simon Mnkondya ameahidi kutoa zawadi ya Nguruwe mmoja mkubwa aina ya Large White mwenye kilo 500 sawa na shilingi Milioni 3 kwa kila goli litakalofungwa na Simba SC katika mchezo wake na Ihefu SC kesho Jumamosi Aprili 13,2024 katika uwanja wa Iliti Singida.



Ahadi hiyo ya Mkondya ambaye ni mdau mkubwa wa michezo imekuja siku chache tu baada ya juzi kutoa ahadi ya kuwapa Dodoma Jiji Nguruwe ama shilingi laki saba kwa kila goli ambalo wangelifunga dhidi ya Yanga Sc lakini bahati mbaya hawakufunga hivyo kukosa zawadi hiyo.

"Juzi nilitoa ahadi ya kuwapa Dodoma Jiji Nguruwe mwenye thamani ya shilingi laki saba kwa kila goli ambalo wangelifunga dhidi ya Yanga Sc bahati mbaya hawakufunga hivyo kukosa zawadi hiyo nawapa pole sana.

Sasa mimi pia ni shabiki wa timu ya Simba Sports Club, na timu yetu kwa sasa inapitia wakati wa ngumu wa upatikanaji matokeo tumefungwa mechi tatu mfululizo na Al Ahly nje ndani na kutolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, pia tukafungwa na Mashujaa na kutolewa katika michuano ya Shirikisho Tanzania hii ni aibu kwetu",amesema Mnkondya.




"Sasa ili kuwapa motisha katika mchezo wa kesho dhidi ya Ihefu ama kama inavyofahamika sasa kama Singida Black Stars mimi na Kampuni yangu tunaahidi kutoa Nguruwe mmoja mkubwa aina ya Large White mwenye kilo 500 kwa kila goli litakalofungwa na Simba katika mchezo huo au kiasi cha Tsh. Milioni 3 ambayo ni thamani ya Nguruwe huyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso