YANGA WATOA SARE NA MAMELODI KWA MKAPA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 31 March 2024

YANGA WATOA SARE NA MAMELODI KWA MKAPA


KLABU ya Yanga imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani mara baada ya kulazimishwa sare na Mamelodi Sundowns 0-0.



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam, Mamelodi waliweza kuutawala mchezo katika kipindi cha kwanza ambapo walitawala kwa asilimia 73% kwa 23% licha ya Yanga Sc kuwa na mashuti matatu yaliyolenga lango huku Mamelodi wakiwa wamepiga moja tu.


Kipindi cha pili Yanga walibadilika na kuonesha hali ya kulitaka bao la kuongoza bila mafanikio licha ya kupata nafasi za wazi nyingi.


Sifa za kipekee zimuendee mlinda mlango wa kimataifa wa Afrika Kusini, Ronwel Williams ambaye aliokoa hatari nyingi ambazo zilitengenezwa na Yanga Sc.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso