WAANDISHI WA HABARI WAWILI WAFARIKIDUNIA KWA AJALI YA GARI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 26 March 2024

WAANDISHI WA HABARI WAWILI WAFARIKIDUNIA KWA AJALI YA GARI


Waandishi wa habari wawili wa mkoa wa Lindi wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea jana usiku wa kuamkia leo Machi 26, 2024 katika eneo la Nyamwage mkoani pwani.


Wanahabari hao walikuwa wanatokea jijini Dar es Saalam kuelekea mkoani Lindi ambapo walipata ajali saa saba usiku leo hilo.


Akizungumza na Mwananchi Digital kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa kipolisi Rufiji, SACP Protas Mutayoba amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori eneo la Nyamwage.


"Waliofariki ni mwandishi wa habari wa kampuni ya Sahara Media group, Josephin Kibiriti na Abdalah Nanda wa Channel Ten na mtu mmoja amejeruhiwa aliyekuwemo ndani ya gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Mziray Abedi, mkazi wa Lindi,"amesema RPC Mutayoba.


Amesema kuwa miili ya marehemu hao imehifadhiwa kwenye Kituo cha afyà Ikwiriri pamoja na majeruhi huyo anaendelea kupata matibabu kwenye kituo hicho.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso