VITUO VYA KISASA UKAGUZI WA MAGARI KUJENGWA MIPAKANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 9 March 2024

VITUO VYA KISASA UKAGUZI WA MAGARI KUJENGWA MIPAKANI

Katika kuhakikisha ajali za Barabarani zinapungua kama sio kuisha kabisa, jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Viwango Nchini (TBS) litajenga vituo maalumu vya ukaguzi wa magari maeneo yote ya mipakani ambapo itafungwa mitambo ya kisasa kwa ajili ya ukaguzi huo.





Hayo yamesemwa na Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi wakati alipofika katika Wilaya ya Longido mkoani Arusha kwa ajili ya kukagua eneo ambalo limetolewa na Wakala wa Barabara (TANROAD) ambako kituo hicho kitajengwa kwa Mkoa wa Arusha.



Kamanda Ng’anzi amebainisha kuwa vituo hivyo vitatumika kukagua magari yote ambayo yanaingia Nchini toka nchi jirani kwa ajili ya kukagua ubora wa magari hayo ambapo yale mabovu hayataruhusiwa kuingia hadi yatakapotengenezwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso