VIJANA KUWENI CHACHU YA KULETA MAENDELEO – RC MACHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 19 March 2024

VIJANA KUWENI CHACHU YA KULETA MAENDELEO – RC MACHA





Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha.



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha amesema vijana ni nguvu kazi ya Taifa hivyo wana wajibu mkubwa wa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuchangia katika ustawi na Maendeleo ya Mkoa na Taifa

Ametoa kauli hiyo march 18 kwenye hafla ya kujitambulisha iliyofanyika kwenye hotel ya karena Mjini Shinyanga,ambayo imetanguliwa na makabidhiano ya ofisi, ikiwa ni siku chache baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga kufuatia uteuzi uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

RC Macha amewataka vijana kujikita katika shughuli za kuwaletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kutumia vyema fursa zinazojitokeza mbele yao kuleta tija na ufanisi,badala ya kujihusisha na makundi mabaya ikiwemo kucheza michezo ya kubahatisha (kamali)

Amesema serikali itaendelea kuwahakikisha kuwepo kwa mazingira ya Amani,usalama na upatikanaji wa huduma bora na stahiki za kijamii,uzingatiwaji wa misingi ya utawala bora,haki na utu kwa wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu huyo wa Mkoa ameonya tabia ya baadhi ya watendaji kujihusisha na masuala ya kisiasa ambapo amesema kwa kufanya hivyo ni kubeba majukumu yasiyowahusu,na badala yake amewataka kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.

Amesisitiza viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi kwa umoja,mshikamano na ushirikiano wa dhati mazingira ambayo yatasaidia kuwaepusha na mianya ya chuki,na migogoro

Anamringi Macha amewataka viongozi na watendaji kutoka ofisi na kwenda kusikiliza kero za wananchi zikiwemo zile za migogoro ya ardhi

Akizungumza katika hafla hiyo naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano Bi Christina Mndeme ameomba viongozi wa Dini, serikali,vyama vya Sasa, taasisi za serikali na sekta binafsi, wadau wote wa Maendeleo na wananchi kumpatia ushirikiano Mkuu huyo wa Mkoa ili kuendelea kuchochea ukuaji wa Uchumi na Maendeleo.

Mndeme amewaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kushiriki vema kwenye ajenda ya kitaifa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuendelea kutunza mazingira.




Anamringi Macha anakuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akichukua nafasi ya Christina Mndeme ambaye amekuwa naibu katibu Mkuu ofisi ya Makamu wa Rais mazingira na Muungano,na kwamba kabla ya uteuzi huo alikuwa naibu katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso