SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA WAOMBA USHIRIKIANO BAINA YAO NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 March 2024

SMAUJATA MKOA WA SHINYANGA WAOMBA USHIRIKIANO BAINA YAO NA HALMASHAURI YA WILAYA YA MSALALA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kampeni ya kupinga ukatili Nchini SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga imeiomba Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kuendelea kushirikiana ili kupunguza au kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika jamii.

Hayo yamebainishwa na viongozi wa SMAUJATA katika kikao cha pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kilicholenga kuwatambulisha viongozi wa SMAUJATA Halmashauri hiyo.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya pamoja na Mwenyekiti idara ya itifaki, uachama na uenezj Bwana Solomon Najulwa wameomba ushirikiano kati ya SMAUJATA na viongozi wa Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bwana Daniel Joseph pamoja na Katibu wa SMAUJATA Halmashauri hiyo Bi. Nives Nyoni wameahidi kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa bidii ili kufikia malengo.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya akizungumza kwenye kikao hicho.

Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.
Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bwana Daniel Joseph akizungumza kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bwana Daniel Joseph akizungumza kwenye kikao hicho.

Katibu wa SMAUJATA Halmashauri hiyo Bi. Nives Nyoni akizungumza kwenye kikao hicho.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge akiwapongeza viongozi wa SMAUJATA huku akiwahakikishia ushirikiano katika kupambana na vitendo vya ukatili.

Viongozi mbalimbali wa SMAUJATA.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga na viongozi wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiwa kwenye picha ya pamoja na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge baada ya kikao.

Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Daniel Kapaya wa kwanza upande wa kushoto, Mwenyekiti idara ya itifaki, uachana na uenezi SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga Bwana Solomon Nalinga upande wa kulia wakiwa kwenye picha ya pamoja na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge.

Viongozi wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakiwa kwenye picha ya pamoja na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge.

Mwenyekiti wa SMAUJATA Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Bwana Daniel Joseph wa kwanza upande wa kushoto, Katibu wa SMAUJATA Halmashauri hiyo Bi. Nives Nyoni wakiwa kwenye picha ya pamoja na kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Bwana Abdulikadri Mfilinge.

Viongozi wa SMAUJATA Mkoa na Halmashauri ya Wilaya ya Msalala wakifanya matembezi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso