RAIS DKT. SAMIA APONGEZWA KUENDELEZA MIRADI YA KIMKAKATI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 20 March 2024

RAIS DKT. SAMIA APONGEZWA KUENDELEZA MIRADI YA KIMKAKATI

Rais Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongezwa kwa juhudi kubwa anazozionesha za kuruhusu kuendelea ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo inayotekelezwa na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya     Ustawi na   Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq,


Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq, wakati wajumbe wa kamati hiyo walipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa hoteli ya nyota tano inayomilikiwa na NSSF iliyopo Jijini Mwanza, tarehe 18 Machi, 2024.


Naye, Mhe. Mwita Getere (Mb), amesema NSSF ina nidhamu ya hali ya juu hasa katika kutekeleza miradi ya uwekezaji ukiwemo wa hoteli ya nyota tano iliyopo Jijini Mwanza.


“Nimpongeze sana Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mradi huu ulikuwa umesimama kwa muda mrefu, lakini alipoutembelea mwezi Juni 2023, aliwatia moyo na kuwataka NSSF waendelee na mradi huu, akijua utakuwa na tija kwa wananchi wa Mwanza na mikoa ya jirani na kuongeza mapato kwa Serikali,” amesema Mhe. Fatuma.




Mhe. Mariam Kisangi (Mb) amempongeza Rais, Dkt. Samia kwa kuhakikisha miradi iliyosimama inatekelezwa na kuwa mradi huo wa hoteli utaleta manufaa kwa NSSF, jamii na Taifa kwa ujumla.


Akitoa taarifa ya mradi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amemshukuru Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye aliridhia mradi huo uendelee baada ya kusimama kwa muda mrefu.




Mhe. Profesa Ndalichako amesema mradi huo ulianza tarehe 1 Novemba, 2013 na ulipangwa ukamilike ndani ya miaka  mitatu, lakini kutokana na changamoto mbalimbali zilizotokea mradi utakamilika tarehe 30 Desemba, 2024.


Naye, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Patrobas Katambi, amewashukuru wajumbe wa kamati hiyo kwa maoni na michango yao ambayo wameichukua na wataenda kuyafanyia kazi.


Pia  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja, amesema upo mpango wa kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza ili iwe rahisi watalii kupita kwa wingi na kuiwezesha hoteli hiyo kupata wageni wengi


Kwa upande wake  Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw. Masha Mshomba  amesema Mfuko unaendelea kutekeleza majukumu yake mbalimbali, ambapo kwa upande wa ulipaji wa mafao ya wanachama, wanalipa kiasi kikubwa zaidi ya kile ambacho mwanachama amechangia na ndio maana wanafanya uwekezaji wenye tija.

 




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso