POLISI KUENDELEA KUWABANA WANAVUNJA SHERIA,WANANCHI WANAOMBA OPERESHENI 3D IENDELE - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 19 March 2024

POLISI KUENDELEA KUWABANA WANAVUNJA SHERIA,WANANCHI WANAOMBA OPERESHENI 3D IENDELE

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Kimeendelea na operesheni ya kutoa elimu na kuwakamata wale wote wanaoendelea kuvunja sheria za usalama Barabarani huku Jeshi hilo likiwapongeza wale wote waliotii agizo la serikali la kuondoa namba ambazo hazijasibitishwa na mamlaka ya viwango Tanzania (TBS).


Akiwa katika Operesheni hiyo leo Machi 19, 2024 Mkoani Arusha Mkuu wa Operesheni za kikosi cha Usalama barabarani Nchini kamishna msaidizi wa Polisi ACP Nasoro Sisiwayah amesema kikosi hicho kinaendelea kuwakamata wale wote walio kaidi agizo la kuondoa namba zenye ujazo 3D na ving’ora.


ACP Sisiwayah ameongeza kuwa operesheni hiyo imelenga pia kukamata madeni ya wale wote waliofanya makosa barabarani na kupigwa faini ambapo amebainisha kuwa zoezi hilo linaendela nchi nzima huku akiwaomba watumiaji wa vyombo vya moto ambao wanadaiwa kuhakikisha wanalipa madeni yao kwa wakati.


Aidha amesema kuwa operesheni hiyo pia imehusisha kuwakamata wale wote wanaoendesha mwendo kasi vyombo vya moto ambapo amebainisha kuwa uchunguzi wa Jeshi hilo unapofanyika umebaini kuwa chanzo cha ajali nyingi ni mwendo kasi hivyo nao watakamatwa.


Nao baadhi ya madereva licha ya kupongeza operesheni hiyo wamebainisha kuwa undoshaji wa namba hizo utasaidia katika swala la ulinzi na usalama huku wakiliomba Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani kuendelea na operesheni hiyo ambayo itasaidia katika usalama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso