NDEGE ZAGONGANA ANGANI WAWILI WAFARIKI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 5 March 2024

NDEGE ZAGONGANA ANGANI WAWILI WAFARIKI

Watu wawili wamekufa kufuatia ajali ya ndege mbili zilizogongana angani na kuangukia katika mbuga ya kitaifa Nairobi, Kenya.


Waliofariki wanaripotiwa kuwa rubani mwanafunzi na mkufunzi waliokuwa ndani ya ndege aina ya Cessna mali ya Ninety-Nines Flying School.


Ndege ya pili, Dash 8, ni ya Safarilink Aviation Limited, ambayo imethibitisha kuwa ilikuwa ikielekea Diani ikiwa na abiria 39 na wafanyakazi watano ilipata kishindo mara baada ya kupaa. Hakuna vifo vilivyoripotiwa kutoka katika ndege hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso