MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA ACHARUKA FEDHA ZA TASAF KUTAFUNWA NA WATUMISHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 March 2024

MWENYEKITI WA CCM MKOA WA SHINYANGA ACHARUKA FEDHA ZA TASAF KUTAFUNWA NA WATUMISHI

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM  Mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa  ameitaka  Halmashauri  ya Msalala Wilayani Kahama Kuhakikikisha inarejesha kiasi cha Sh,Milioni  16 wanazirejesha kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF  kwenye Halmashauri hiyo.



Mwenyekiti  wa CCM Mabala Mlolwa ameoneshwa kuchukizwa na kitendo kilichofanywa na watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kutafuna fedha za wanufaika wa mfuko wa maendelo ya jamii TASAF jambo ambalo ni kinyume cha Sheria.


“Kusimamishwa watumishi sio kigezo  tunachotaka ni pesa irudishwe yani kweli unakula pesa ya mtu masikini uoni hata aibu kabisa harafu Kaimu Mkurugenzi unakuja unatuambia eti umewasimamisha watumishi hii kauli sikubaliani nayo Mpigie simu Mkurugenzi mtendaji wa Msalala Mwambie Mwenyekiti anataka pesa ya wanufaika wa TASAF ilipwe sikubali kuona uonevu wa kwa wananchi” amesema Mabala




Mwenyekiti  huyo  amemuagiza  
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kufikia  ijumaa ziwe zimerudishwa.


Kufuatia maelekezo hayo Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Mfilinge Abdullah amesema wanaendelea na juhudi ya kuhakikisha fedha hizo wanazirudisha kwa wananchi na tayari watumishi ambao wameonekana kwenda kinyume na fedha hizo wameshasimamishwa kazi.


“Ndugu  Mwenyekiti nikuhakikishie  kuwa kiasi cha Milioni 16 ambazo zimebakia tutahakikisha tunazirudisha kwa wakati kwa wanufaika wa mfuko wa TASAF tunaomba mtusamehe tu kwani tayari tunaendelea na mchakato wa Malipo ya Fedha zote zinazodaiwa”  amesema  Mfilinge Abdulllah, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala


Naye  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Msalala, Mibako Mabubu amemuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Kuhakikisha ifikapo Ijumaa ya wiki hii  pesa  zote zitakuwa zimefika kwa walengwa. 


Kwa  upande wake  Mbunge  wa Msalala  Iddi  kassim Iddi ameahidi kushughulika na watu ambao wataonekana kudhurumu haki za wananchi.



Chanzo : FullShangwe

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso