MUUNDO MPYA UEFA WATANGAZWA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 March 2024

MUUNDO MPYA UEFA WATANGAZWA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) limetangaza muundo mpya wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa msimu wa 2024/2025.


Awali zilikuwa timu 32 na sasa zitaongezeka hadi 36.


Kutakuwa na poti nne, kila timu itakuwa na michezo minne ya nyumbani na minne ugenini, hivyo kila timu itakuwa na michezo minane.


Timu ambazo zitamaliza nafasi ya 1-8 zitaenda moja kwa moja 16 bora, timu ambazo zitashika nafasi ya 9-24 zitashindana zenyewe kwenye mtoano.


Timu zitakazoshika nafasi ya 25-36 zitaondolewa moja kwa moja kwenye mashindano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso