Mji wa Port-au-Prince wakumbwa na mashambulizi mapya - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 21 March 2024

Mji wa Port-au-Prince wakumbwa na mashambulizi mapya


Magenge ya watu wenye silaha yameanzisha mashambulizi mapya nchini Haiti, na kutokana na hali hiyo Marekani imeanza kuwahamisha raia wake kutoka nchini humo.Milio ya risasi imesikika katika viunga vilivyo karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Port-au-Prince, maeneo ambayo yalikuwa na utulivu.



Wanahabari wa shirika la Habari la Associated Press wameripoti kuiona takriban miili mitano walipozunguka kwenye baadhi ya vitongoji, ingawa magenge ya wababe yameweka vizuizi kwenye baadhi ya maeneo na kuwafanya waandishi hao wa habari kushindwa kufika kwenye maeneo hayo.


Watu katika maeneo yaliyokumbwa na mashambulizi walipiga simu vituo vya redio wakiomba msaada kutoka kwa jeshi la polisi ambalo lenyewe limesalia na maafisa wachache ambao wanazidiwa nguvu na magenge ya watu wenye silaha wanoudhibiti mji mkuu wa Haiti

Gavana wa Florida Ron DeSantis, amesema anaelewa kuwa kuna wamarekani walio hatarini. Gavana huyo wa Florida Ron DeSantis amesema zaidi ya wamarekani 300 kutoka kwenye jiji hilo wako nchini Haiti, na operesheni hiyo ya kuwahamisha inayofadhiliwa na jiji la Florida itaendelea licha ya kukabiliwa na ukiritimba kutoka kwa serikali kuu ya Marekani na pia vitisho vya usalama nchini Haiti.

Maafisa wa Haiti wanajitahidi kufanikisha kuundwa baraza jipya la mpito litakalo kuwa na jukumu la kumteuwaWaziri Mkuu wa mpito na baraza lake la mawaziri.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso