MIOYO YA WATANZANIA IMEGUBUKWA DHULMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 5 March 2024

MIOYO YA WATANZANIA IMEGUBUKWA DHULMA


''Katika mikoa 23 niliyotembea kwa awamu zote mbili, nimebaini dhulma katika sekta ya ardhi unayofanywa na matajiri na baadhi ya watumishi wa umma imesababisha mioyo mingi ya Watanzania kugubikwa na dhulma na hivyo kuichukia Serikali yao'' amesema makonda.






''Wananchi wengi wanalalamikia wenye nazo na makamisha wa ardhi na wapimaji kuwadhulumu ardhi yao huku wengine wakitoa hati juu ya hati'' amesema makonda.


''Chama kinamwagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa kufanya mapitio ya wafanyakazi wote wanaotajwa kuwa kwenye mtandao wa dhulma sekta ya ardhi ili watakaobainika wachukuliwe hatua za kisheria'' amesema makonda.


Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CCM Paul Makonda amesema hayo wakati akitoa tathmini ya ziara yake ya kutembelea mikoa 23 kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kusikiliza kero za wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso