CUBA NA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 6 March 2024

CUBA NA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA MAENEO YA KIMKAKATI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Cuba, nchini Tanzania, Mhe. Yordenis Despaigne Vera. Katika Mazungumzo hayo Dr. Nchimbi na Mhe. Balozi Vera wamejadiliana juu ya masuala mbalimbali yanayohusu namna ya kuimarisha zaidi uhusiano kati ya Tanzania na Cuba na Chama Cha  Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha Cuba (CPC).


 Katibu  Mkuu  wa  Chama  Cha  Mapinduzi (CCM)  Balozi Dk. Emmanuel  John  Nchimbi  akizungumza  na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania Mhe. Yordenis Despaigne Vera, walipokutana  kwa  ajili  ya  mazungumzo 


Wakati wa Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya  CCM, Lumumba  jijini Dar Es Salaam, Machi 5, 2024, Mhe. Balozi Vera ameishukuru Tanzania  na CCM kwa jinsi ambavyo daima wamesimama na nchi hiyo katika nyakati zote.


Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CCM  Balozi Dk. Nchimbi amemhakikishia Mhe. Balozi Vera kuwa CCM  chini ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan  kitafanya kila linalowezekana kuhakikisha urafiki na uhusiano kati ya Tanzania na Cuba kwa upande mmoja na CPC na CCM kwa upande mwingine unaenziwa na kuimarishwa zaidi kwa ajili ya manufaa ya pande zote mbili.



Kupitia majadiliano hayo  pamoja  na  masuala mengine viongozi hao wa pande zote mbili   wamejadiliana na kuainisha maeneo yatakayofanyiwa kazi kwa ajili ya kuboresha na kuimarisha ushirikiano kati ya Wananchi wa Tanzania na Wananchi wa Cuba, Serikali za nchi zote mbili na vyama vinavyoongoza nchi hizo, huku wakisisitiza umuhimu wa kuendeleza mipango ya kubadilishana utaalam katika maeneo mbalimbali na kuimarisha ushirikiano katika maeneo ya kiuchumi.



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso