AJIFUNGUA MAPACHA WATATU AOMBA MSAADA-GEITA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 8 March 2024

AJIFUNGUA MAPACHA WATATU AOMBA MSAADA-GEITA

Rebeka John (27), mkazi wa Ikurwa Wilaya ya Geita amejifungua watoto watatu njiti Machi 04, 2024 katika Kituo cha Afya Nyankumbu kilichopo Mjini Geita ameomba wasamaria wema wamsaidie ili aweze kupata mahitaji ya watoto, hasa maziwa.



Mama huyo ambaye pacha wake wapo chini ya uangalizi maalumu kutokana na wao kuzaliwa na uzito pungufu, amesema changamoto kubwa aliyonayo kwa sasa ni maziwa na nguo.


Mwanamke huyo ambaye anao watoto wengine watano, amesema hakutarajia kujifungua watoto watatu kwani wakati wote aliohudhuria kliniki hakuelezwa kama amebeba watoto watatu tumboni.


Pia amesema mume wake ni mkulima ambaye na hana uwezo.


Mganga Mfawidhi kituo cha Afya Nyankumbu Irene Temba amesema hali ya mama inaendelea vizuri lakini changamoto aliyonayo ni maziwa kutoka kidogo yasiyowatosheleza watoto na yeye anapaswa kuzingatia lishe bora ili watoto wapate maziwa ya kutosha.


Kwa atakaeguswa kumsaidia mama huyo atumie namba 0762 163 961 ambayo ni ya mumewe Daudi Mtenya.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso