SOKO LA MBUYUNI MOSHI LATEKETEA KWA MOTO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 7 February 2024

SOKO LA MBUYUNI MOSHI LATEKETEA KWA MOTO

 Soko  la Mbuyuni manispaa ya Moshi  mkoani Kilimanjaro limeteketea kwa moto na kuacha wafanyabiashara zaidi ya 2500 wakiwa hawajui la kufanya baada ya bidhaa  zao zote kuteketea.


               Soko  la Mbuyuni manispaa ya Moshi 

Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  Suki , na Mjumbe wa Kamati Kuu  ya CCM  Rabia Abdallah Hamid

Moto huo ulioanza kuwaka majira ya saa sita usiku wa kuamkia leo na chanzo chake bado hakijajulikana ambapo moto huo umesababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara hao ambao asilimia kubwa wanaendesha biashara kwa mikopo.


Akizungumza mara baada ya kutembelea soko hilo na kujionea hasara hiyo, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Suki , na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Rabia Abdallah Hamid amesema kuwa chama cha Mapinduzi kitaenda kuongea na taasisi za benki ambazo zimewakopesha wafanyabiashara wa soko hilo ili kuhakikisha hawanyanyasiki katika kurudisha mikopo yao.


“Viongozi mnapaswa muanze mara moja kuwatambua ni wafanyabiashara wangapi ambao walikuwa na mikopo na asiachwe hata mmoja kwani kuna utaratibu wa kurejesha marejesho kila mwezi lakini kwenye hili sisi chama cha Mapinduzi tutaenda kukaa na taasisi hizo ili kuhakikisha wafanyabiashara hawa hawanyanyasiki katika kipindi hiki” alisema Rabia

Chanzo : Michuzi Blog

 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso