NJIA 4 ZAANZA KUPANULIWA MLIMA KITONGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 1 February 2024

NJIA 4 ZAANZA KUPANULIWA MLIMA KITONGA

Hatimaye kilio cha muda mrefu cha Watumiaji wa barabara kuu ya TANZAM kutokea Ruaha Mbuyuni hususani eneo la mlima Kitonga kimeanza kufanyiwa kazi kwa kupanua barabara hiyo kuifanya ya njia nne ili kuepusha foleni za mara mara na kuufanya mlima huo kupitika kiurahisi.
                                   

Meneja wa TANROADS mkoa wa Iringa Mhandisi Yudas Msangi amesema ujenzi wa mradi huu utagharimu shilingi bilioni 6.4 hadi kukamilika kwake.


Amesema barabara hiyo itajengwa kwa kiwango ya njia nne ambayo itakuwa na mifereji mikubwa ya kuongoza maji na kufungwa vioo vikubwa kwenye kila kona ili kusaidia upishano mzuri wa magari nyakati zote.
 
Chanzo:MillardAyo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso