NGOs ZATAKIWA KWENDA KUHUISHA MIKATABA YAO INAPOISHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 1 February 2024

NGOs ZATAKIWA KWENDA KUHUISHA MIKATABA YAO INAPOISHA

Kutokana na chamgamoto mbalimbali zinazoyakabiri mashirika yasiyo ya kiserikali likiwemo suala la ukomo wa kutoa huduma, Msajili wa mashirika hayo Vickness Mayao amesema kuwa suala hilo ni la kawaida hivyo wanatakiwa kwenda kuhuisha miakataba yao ili yanaendelee kutoa huduma.



Na Gideon Gregory, Dodoma.

Bi. Mayao ameyasema hayo leo Januari 31,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi cha mitandao mbalimbali inayofanya kazi ya kuleta maendeleo nchini na wizara ya maendeleo ya jamii jinsia, wanawake na makundi maalumu.


“Kwahiyo napenda kutoa rai na kuyahakikishia mashirika haya kuwa hakuna shirika litakalo futiwa kwasababu ukomo umefika kwahiyo tutaendelea kutambua michango yao hata kama miaka 10 ya kutoa huduma ikifika,” amesema.


Aidha Bi. Mayao ameyataka mashirika hayo kuhakikisha yanaandaa miradi ambayo ni endelevu ili kuweza kujipatia fedha za kuendesha mashirika yao kuacha kutegemea fedha kutoka kwa wahisani.


“Tunajaribu kuangalia kama itawezekana hata kama ni kwa udogo wake kuwa na mfuko mdogo utakao mashirika haya kwanza lakini tayari serikali imekwisha anza kuyasaidia baadhi ya mashirika madogo hapa nchini,”amesema.


Naye Mkurugenzi wa mtandao wa mashirika binafsi (TANGO) Adamson Msimba ametaja lengo la kufanya kikao hicho huku akiipongeza serikali kwa kuendelea kuwathamini kwa huduma wanazozitoa.


Akizungumza kwa niaba ya wenzake waliohudhuria katika kikao hicho kutoka hasasi za kiraia Mkoa wa Dodoma Edward Mbogo amesema wanafanya kazi kwa ukaribu na serikali huku akiongeza kuwa suala la teknolojia limekuwa likileta mkanganyiko katika ulipaji wa kodi kwa mashirika hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso