MTOTO WA MIAKA 7 AUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI- BABATI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 21 February 2024

MTOTO WA MIAKA 7 AUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI- BABATI

 

Mtoto mdogo mwenye miaka 6 Mpaka 7  mwanafunzi wa darasa la awali shule ya msingi  Mapea kata ya Magugu wilayani Babati mkoani Manyara   Maria Chacha  ameuawa kwa kuchinjwa na kutenganishwa kichwa na kiwiliwili kisha kutupwa mtoni  kwenye mashamba ya wawekezaji.


Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji cha Mapea  Ndg Filemon Mbogo, amesema  tukio hilo la kusikitisha na la kutisha limetokea februari 20,2024 ambapo mtoto huyo Maria Chacha akiwa na wenzake wakiwa wanatoka shule walikutana na mtu ambaye aliwataka waongozane naye kwenda kuchuma matunda aina ya mazambarau na walipofika mbele wenzake waliona ni mbali wakaamua kugeuka  lakini mtu huyo alimbeba Maria na kuondoka naye.


Amesema wazazi wa mtoto huyo walibaini tuko hilo baada ya kupata taarifa kutoka kwa wenzake waliokuwa wameongozana pamoja wakitoka shule ndipo wakatoa taarifa katika uongozi wa kijiji na wananchi kuanza kumtafuta saa saba mchana na baadae waliukuta mwili wa mtoto huyo katika shamba la mwekezaji  Odedra eneo lenye mto na  vichaka vikubwa pamoja na miti aina ya mikuyu.


 

Mbogo amesema mtoto huyo alichinjwa shingoni  kisha kiwiliwili kikatupwa kwenye mto na kuwekewa gogo juu huku kichwa kikiwa pembeni .Pia ameeleza  kuwa tukio hilo sio la kwanza kutokea kwani katika maeneo hayo ilishapatikana miili miwili na mpaka sasa mtoto mwingine haijulikani alipo kwa zaidi ya miezi mitatu


Kamanda wa Polisi mkoani Manyara George Katabazi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akiwataka wananchi waendelee kuwaripoti wahalifu na kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao


Mpaka sasa hakuna taarifa za mtu kushikiliwa na jeshi la Polisi kutokana na mauaji hayo.

 


Chanzo :FullShangwe

 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso