WACHIMBAJI MGODINI HAWAJAONEKANA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 December 2023

WACHIMBAJI MGODINI HAWAJAONEKANA



MAOFISA nchini Zambia wameshindwa kupata makumi ya wachimbaji haramu wanaoaminika kunaswa baada ya maporomoko ya udongo kwenye mgodi wa shaba Ijumaa.


Ajali hiyo ilitokea katika jimbo la Kaskazini la Copperbelt nchini humo baada ya mvua kubwa kunyesha.


Vikosi vya uokoaji vimekuwa vikivuta maji kutoka kwenye mashimo ya chini ya ardhi kwenye mgodi wa Sesili uliopo Chingola lakini hawakuwapata na wachimbaji hao.


Rais Hakainde Hichilema alisema amesikitishwa na “hali hiyo ya kuhuzunisha”. Makamu wa Rais, Mutale Nalumango alisema tukio lililotokea katika mgodi wa Sesili ni janga.

Chanzo: habarileo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso