VIFO VYAONGEZEKA MKOANI MANYARA KUTOKANA NA MAFURIKO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 December 2023

VIFO VYAONGEZEKA MKOANI MANYARA KUTOKANA NA MAFURIKO

Wakati vifo vilivyosababishwa na maporomoko ya matope vikiongezeka na kufikia 49 wilayani Hnang’, askari 350 wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wamewasili kwa ajili ya kusaidia shughuli za uokoaji.


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga ameyasema hayo leo Jumatatu Desemba 4, 2023 wakati akizungumzia kuongezeka kwa vifo hivyo ambavyo idadi jana Desemba 3, 2023 vilikuwa 47.


RC Sendiga amesema vifo vimefika 49 na majeruhi 85 na askari, maofisa wa JWTZ ambao ni wataalamu wa uokoaji wameshafika Hanang' na watashiriki shughuli za uokoaji wa watu waliokumbwa na maafa hayo.


Eneo kubwa lililoathiriwa na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi na Katesh ambapo ndipo makao makuu ya Wilaya ya Hanang’.


Nyumba za watu zimezingirwa na mafuriko na miti iliyosombwa na mafuriko kutoka sehemu ya Mlima Hanang yamesababisha barabara ya Katesh kwenda Singida kushindwa kupitika kwa muda.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kufuatia tukio hilo na kuzitaka mamlaka zote zihamishie nguvu wilayani Hanang kutoa msaada wa haraka.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso