LORI LA KEMIKALI LAUA DEREVA NA KODAKTA KWA KUTUMBUKIA MTONI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 4 December 2023

LORI LA KEMIKALI LAUA DEREVA NA KODAKTA KWA KUTUMBUKIA MTONI


Watu wawili wanahofiwa kufariki dunia baada ya lori walilokuwemo kupoteza mwelekeo na kuingia mtoni kisha kulipuka katika eneo la makutano ya Barabara ya Mwanza- Musoma - Tarime.Picha hii sio halisi ya eneo la tukio


Tukio hilo limetokea leo Jumatatu Desemba 4, 2023 saa 12 asubuhi katika eneo la makutano wilayani Butiama mkoani Mara.


Watu hao ambao ni dereva na kondakta bado hawajajulikana majina yao na sehemu waliyokuwa wanaenda kutokana na kushindwa kutoka nje baada ya gari kutumbukia mtoni na kulipuka.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Salum Morcase amesema gari hilo lilikuwa linatoka Mwanza na kwamba hadi sasa haijajulikana lilikuwa linaelekea wapi.


Amesema kwa mujibu wa uchunguzi wa awali wamebaini kuwepo kwa mapipa ambayo yanadhaniwa kuwa na kemikali ingawa haijajulikana kulikuwa na kemikali za aina gani na zilikuwa zinapelekwa wapi.


"Hizi kemilali ni kama za kwenye migodi, tunafanya mawasiliano na migodi iliyopo hapa Mara ili tuweze kujua zaidi mzigo ulikuwa unaelekea wapi na akina nani walikuwepo kwenye gari," amesema.


Chanzo: Mwanchidigital

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso