SAMAKI WAPANDA BEI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 19 September 2023

SAMAKI WAPANDA BEI


Upatikanaji wa samaki katika Soko la Kimataifa la Samaki Feri Dar es Salaam sio wa kuridhisha kutokana na upepo kuwa mkali baharini.


Ofisa Mwandamizi wa Uvuvi kutoka sokoni hapo, Ramadhan Mtabika amesema hayo wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari.


Amesema upepo unapokuwa mkali baharini unawafanya wavuvi wengi kutokwenda kuvua.


“Hali ya samaki sio nzuri, upatikanaji wake hauridhishi kwa kuwa hali ya hewa inapima upatikanaji wake. Sasa hivi upepo mkali unasababisha wavuvi wengi kutokwenda baharini,” amesema.


Amesema katika hali hiyo ya upatikanaji mdogo wa samaki baharini, dagaa ndio wanaopatikana kwa wingi zaidi.


“Dagaa aina ya mchele ndio wanapatikana kwa wingi kipindi hiki japo si kwa kiwango ambacho wanapatikana kipande kingine,” amesema.


Kwa maelezo yake kwa sasa bei ya dagaa mchele ndoo ya kilo 20 inauzwa Sh 50,000 lakini kabla ya uchache huo ilikuwa Sh 20,000 mpaka 30,000.


Samaki aina ya jodani kwa sasa kilo ni Sh 12,000, tasu ni kilo ni Sh 8000.


Kabla ya msimu huu jodani kilo ilikuwa ni Sh 9000 na 10,000 na tasa ni kati ya Sh 5000 na 6500.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso