MWALIMU MBARONI KWA KUMNAJISI MWANAFUNZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday 20 September 2023

MWALIMU MBARONI KWA KUMNAJISI MWANAFUNZI


JESHI la polisi mkoani Mtwara linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi ya Mkalapa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kumnajisi mwanafunzi wa darasa la saba.


Mwalimu huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi inadaiwa alitenda tukio hilo mwishoni mwa wiki iliyopita.


Kwa mujibu wa mwanafunzi huyo mwalimu huyo alimwambia afuate madumu ya maji aliyoyaacha nyumbani kwa mwalimu huyo wakati wa kumaliza mtihani wake wa darasa la saba na kisha kumlazimisha kumwingilia kimwili.


Mwalimu anayedaiwa kufanya tukio hilo ni wa kujitolea na anaishi katika moja ya nyumba ya shule iliyopo katika eneo hilo.


Kwa upande wa wazazi na walezi wa mtoto huyo wamesema kwa kuwa uthibitisho umekamilika wanasubiri tamko la jeshi la polisi kumfikisha mahakamani.


Baada ya kutendewa tukio hilo, alipelekwa katika hospitali ya St. Benedict ya Ndanda kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso