WATANZANIA WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 17 August 2023

WATANZANIA WAHIMIZWA KUTEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA



Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kutoa wito kwa Watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea Makumbusho ya MajiMaji iliyopo katika Manispaa ya Songea kwani ni Makumbusho iliyosheheni historia ya Muafrika pamoja na mikusanyo mbalimbali ambayo haipatikani sehemu yoyote isipokuwa katika Makumbusho hiyo.


Wito huo umetolewa na Afisa Elimu wa Makumbusho hiyo Rose Kangu ambapo amesema bado kuna kazi ya kuendelea kuwaelimisha Watanzania ili waweze kuijua historia ya kipekee ambayo inapatikana katika Makumbusho hiyo.


Imeelezwa kuwa Makumbusho hiyo inatumika kuhifadhi na kuonesha historia ya Vita vya Maji Maji vilivyotokea mwaka 1905 -1907, na ni moja kati ya Makumbusho ambayo ipo katikati ya Mji wa Songea.


Kangu amesema kutembelea katika Makumbusho hiyo kwanza unapata historia ya vita vya Majimaji pia utajifunza jinsi mababu zetu walivyopambana na Wakoloni kwa kutumia mbinu mbalimbali ili kukinda Utu na heshma yetu hivyo kizazi cha sasa kinapaswa kutumia mbinu ya Utu, Utaifa, Mshikamano katika kupambana na ukoloni mamboleo.


“Wadau wetu wakubwa wamekuwa ni wanafunzi wanaokuja kuitembelea Makumbusho hii, Ni kizazi ambacho tunakihitaji sana kwani wao ndio watakuwa wadau wakubwa wa kurithisha Urithi huu kwa kizazi Kijacho, Kama tunavyojua sisi Makumbusho ya Majimaji tunatunza historia adhimu ya vita vya Majimaji lakini pia Hifadhi vielelezo vya utamaduni wa muafrika.”amesema.


Aidha, Bi. Kangu ametoa wito watu Mbalimbali wakiwa na familiza zao kuitembelea Makumbusho hiyo kwani licha kupata Burudani, wataweza jifunza historia adhimu ya Mashuja wa Vita hiyo iluyopiganwa Kwa muda mrefu zaidi Barani Afrika na faida za kuenzi Utamaduni wetu.


Kwa upande wake Kalebi Christopher mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM ) anayesoma Kitivo cha Utalii na Utamaduni aliyekwenda kwa ajili ya mafunzo amewashauri wanafunzi wenzake wa vyuo, sekondari, shule za msingi kwenda kutembelea Makumbusho hiyo kutokana na kuwepo kwa vitu vingi vya kujifunza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso