WALIOSHAMBULIA WANDISHI WA HABARI KUSAKWA USIKU NA MCHANA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 17 August 2023

WALIOSHAMBULIA WANDISHI WA HABARI KUSAKWA USIKU NA MCHANA

MKUU wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amelaani tukio la wanahabari kushambuliwa na kujeruhiwa na baadhi ya vijana jamii ya kifugaji walipokuwa wakitekeleza majukumu yao eneo la Enduleni ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngororongoro (NCAA).


Kutokana na hali hiyo ameliagiza jeshi la Polisi kukamata watuhumiwa hao na sheria kuchukua mkondo wake bila kujali muhusika ana wadhifa gani.


Akizungumza wakati alipotembelea hospitali ya Fame iliyopo wilayani Karatu, amesema wanahabari hao walikuwa wakitekeleza majukumu yao juzi ya kuzungumza na wafugaji walioamua kuhama kwa hiari kupisha uhifadhi.


Amesema, serikali itawasaka wahusika na kuwachukulia hatua na kwamba mhusika kama ni Mbunge, diwani au wadhifa mwingine wowote atakamatwa tu.


Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Justine Masejo amesema jeshi la polisi tayari limeshafungua jalada la shauri hilo na wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo.


Awali Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Elibariki Bajuta alisema NCAA imesikitishwa na tukio hilo na kutoa rai kwa wanasiasa kuacha uchochezi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso