TCRA KUTENGENEZA KATUNI ZA WATOTO KULINDA MAADILI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday 7 August 2023

TCRA KUTENGENEZA KATUNI ZA WATOTO KULINDA MAADILI


Katika jitihada za kukabiliana na maudhui yasiyofaa Mamlaka ya mawasiliano TCRA imesema inashirikiana na mzalishaji binafsi kutengeneza katuni za watoto.


Suala la kuwepo kwa katuni zisizoendana na maadili ya Kitanzania limekuwa likiibuka na kuzua minong'ono miongoni mwa watu huku TCRA ikirushiwa lawama kwa kutodhibiti maudhui hayo.


"Katika suala la katuni zisizofaa kwa watoto, TCRA kwa kushirikiana na mzalishaji binafsi ili kuzalisha katuni zenye viwango vya juu kwa ajili ya watoto, vilevile tunarekodi michezo ya kitamaduni ya makabila 120 ambayo nayo itakuwa katika ubora wa hali ya juu," alisema Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Jabiri Bakari katika taarifa ya mamlaka hiyo kwa vyombo vya habari.


Dk Jabiri alisema majukumu ya TCRA ni zaidi ya zaidi ya kuwezesha huduma za matangazo kwani mamlaka hiyo inajukumu la kuhakikisha maudhui yanayorushwa yanafuata maadili ya uandishi wa habari, yanazingatia sheria za nchi, kulinda maadili na urithi wa Taifa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso