NFRA WAHIMIZA WAKULIMA KUTUMIA MAGHALA KUHIFADHI CHAKULA NCHINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 8 August 2023

NFRA WAHIMIZA WAKULIMA KUTUMIA MAGHALA KUHIFADHI CHAKULA NCHINI

AFISA mtendaji mkuu wa wakala wa Taifa hifadhi ya chakula NFRA Milton Lupa katika kuhakikisha kuwa usalama wa chakula nchini wana majukumu makubwa matatu ambayo kwanza ni kununua na kuhifadhi chakula na pili ni kutoa chakula wakati wa dharula ama wakati wa majanga yanayojitokeza ndaniya nchi na jukumu la tatu ni kuuza chakula ambacho muda wake wa kuhifadhi umekwisha ili kuweza kununua akiba mpya.



NA PAUL KAYANDA-MBEYA


Amesema kuwa jukumu lingine walilopewa hivi karibuni na serikali ni kuhakikisha kuwa wanadhibiti mfumuko wa bei ambapo pale mahindi yanapokuwa bei ya juu wao wanatoa mahindi kwa bei ya chini ili kusababisha wafanyabiashara wapunguze kwa bei.


AFISA mtendaji mkuu huyo wa wakala wa Taifa hifadhi ya chakula NFRA ameyasema hayo alipokuwa kwenye mahojiano maalumu na vyombo vya habari katika maonesho ya nane nane yanayofanyika katika viwanja vya john Mwakangale jijini Mbeya.


Aidha amesema kuwa kama sehemu ya wizara ya kilimo wapo nane nane kuonyesha wakulima jinsi ya uhifadhi wa mazao na kubainisha kuwa nafaka ambazo kwa sasa wananunua na kuhifadhi ni mahindi, mpunga pamoja na mtama na kuongeza kuwa kwa sasa wamefungua vituo katika kanda zote.


Alifafanua kuwa wananunua kwa bei ambayo ipo juu ya soko ili kuwawezesha wakulima kupata pesa ili waweze kurudui mashambani na kuongeza kuwa mpaka sasa wamenunua tani zaidi ya 75,000 na wanategemea kwamba watanunua tani zaidi ya laki tatu,(300,000).


Pamoja namambo mengine kiongozi huyo amewataka wananchi kuleta mahindi kwa NFRA watanunua kwa bei nzuri lakini pia hata wao wakulima wakileta NFRA watakuwa wamejiwekea akiba kwa sababu likitokea janga lolote la njaa NFRA wataleta chakula.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso