MASHABIKI WA SIMBA WAMALIZA SIMBA DAY KWA KITOWEO CHA NG'OMBE, MSALALA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 8 August 2023

MASHABIKI WA SIMBA WAMALIZA SIMBA DAY KWA KITOWEO CHA NG'OMBE, MSALALA

Mashabiki wa Simba katika kata ya Kashishi, halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama wakiwa na ng'ombe waliochija siku ya Simba Day na kusherekea kwa kula chakula cha pamoja kwa kuwaalika watani wao wa jadi wa timu ya Yanga pamoja na jamii , Picha na Patrick Mabula.

Mbalimbali za matukio ya Mashabiki wa Simba wa kata ya Kashishi , halmashauri ya Msalala , wilayani Kahama walipochinja ng'ombe wawili na kula chakula cha pamoja na watani zao wa Yanga pamoja na jamii ya kata hiyo kwa lengo la kuimalisha upendo, mshikamano na umoja miongoni mwao Picha zote na Patrick Mabula.

Mashabiki wa timu ya Simba katika kata ya Kashishi , halmashauri ya Msalala , wilaya ya Kahama wamesherekea Simba day kwa kuchanga na fedha na kusaidia katika suala la elimu.

Mashabiki hao waliokuwa wameandaa chakula cha pamoja na kuwaalika watani wao wa Yanga na wanajamii wa kata ya Kashishi wachinja kitoweo cha ng’ombe mbili ambapo katika sherehe hiyo walichanga fedha ambazo watazikabidhi katia kusaidia suala la elimu.

Akiongea katika hafla hiyo mmoja wa viongozi wa tawi la simba katika kata hiyo Manungu Mahumbi alisema walamua kusherekea Simba day kwa kuandaa chakula cha pamoja na kuwaalika watani wao wa jadi wa timu ya Yanga pamoja na jamii wanayoishi nayo.

Vumilia Nyerere alisema lengo la kuandaa chakula hicho na kula pamoja ni kuwa siku zote utani wa jadi katika michezo siyo uadui bali na kudumisha urafiki , upendo na mshikamamano miongoni mwao.

“ Chakula tulichoandaa katika kufurahia siku ya Simba day na kula pamoja na watani zetu wa jadi wa Yanga pamoaj na jamii tunayoishi nayo ni kuendeleza urafiki, udungu miongoni mwetu ,, Alisemna Nkuba Aljabili .

Nao mashabiki wa Yanga wakiongea katika hafla hiyo Jidasagula John na Philipo Jackson waliwashukuru watani zao wa Simba kwa mpango huo kwa sababu siku zote utani wa Simba na Yanga kupitia michezo siyo uadui bali ni kudumisha urafiki ,umoja na mshikamano.

Naye Sali Buzali alisema waliona katika kusherekea Simba day wasiishie kula cha kula pekee bali waliamua kuchanga fedha ambazo watazikabidhi katika moja ya shule ya msingi iliyopo kijiji cha Mwamboku ziweze kusaidia katika suala la kutatua sehemu ya changamoto zilizopo hapo zinazowakabili watoto wao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso