WAZIRI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ASUBUHI YA LEO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 2 May 2023

WAZIRI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI ASUBUHI YA LEO



Waziri wa Nchi anayeshughulikia Kazi, Ajira na Mahusiano ya Viwanda nchini Uganda, Kanali mstaafu Charles Okello Engola ameuawa kwa kupigwa risasi asubuhi ya leo na mlinzi wake akiwa nyumbani kwake.


Tukio hilo limetokea leo Mei 2, 2023 jijini Kampala katika Kitongoji cha Kyanja anakoishi waziri huyo ambapo bado chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana.


Naibu msemaji wa polisi wa Kampala, Luke Owoyesigire amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku maofisa usalama wakiimarisha ulinzi katika eneo yalipotokea mauaji hayo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso