MWALIMU AMCHOMA KISU MWALIMU MWENZAKE GEITA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 17 March 2023

MWALIMU AMCHOMA KISU MWALIMU MWENZAKE GEITA

Mwalimu wa Shule ya Msingi Igaka, Samwel Subi anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Geita kwa tuhuma za kumuua mwalimu mwezake Emanuel Chacha (pichani) kwa kumchoma na kisu akiwa darasani.

Mwalimu Chacha Wakati wa uhai wake

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea Machi 15 saa 3:45 asubuhi wakati walimu hao wakiandaa mtihani kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la kwanza.


“Kata ya Isulwabutundwe mwanaume wa miaka 35 katika Shule ya Msingi Igaka aliuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye chembe ya moyo na mwanaume mwingine mwenye miaka 35 ambae ni mwalimu mwenzake. Walimu wote wawili walikuwa darasani wakiandaa mtihani ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma mwenzake kwenye chembe cha moyo,” amesema Kamanda Jongo.

CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso