BASI LA ANGUKIA KWENYE KORONGO MKOANI KATAVI, TISA WAFARIKI AKIWEMO MJAMZITO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 7 March 2023

BASI LA ANGUKIA KWENYE KORONGO MKOANI KATAVI, TISA WAFARIKI AKIWEMO MJAMZITO

Watu tisa wamepoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Kombas kuacha njia na kupinduka kwenye korongo la mlima Nkondwe wilayani Tanganyika.

Baadhi ya majeruhi wakiwa hospitali ya wilaya ya Tanganyika


Ajali hiyo imetokea jana Machi 6 saa 9:45 alasiri ambapo imeelezwa kuwa baada ya kufika eneo la mlima Nkondwe basi hilo liliserereka hadi kwenye korongo hilo lenye kina cha mita zisizopungua 75 chini yake kukiwa na mto.


Mganga Mkuu hospitali ya wilaya ya Tanganyika Daktari Alex Mrema amesema vifo hivyo vimetokea papo hapo, ambapo wanaume walikuwa watano kati yao kulikuwa na mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri miaka miwili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso