WATU 12 WAFARIKI, 50 WAJERUHIWA, AJALI BASI LA FRESTER LINALOFANYA SAFARI ZA BUKOBA KWENDA DAR. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 9 February 2023

WATU 12 WAFARIKI, 50 WAJERUHIWA, AJALI BASI LA FRESTER LINALOFANYA SAFARI ZA BUKOBA KWENDA DAR.



Watu 12 wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester lenye namba za usajili (T 415 DPP) lililokuwa likitokea Bukoba kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori lenye shehena ya saruji.


Ajali hiyo imeripotiwa tokea saa sita usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 katika Kijiji Cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma - Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari.


Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji amefika eneo la ajali na kutoa rai kwa madereva kuzingatia usalama na sheria za barabarani.

CHANZO:(Azam tv)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso