WAHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA KUIBA MAFUTA YA UJENZI WA SGR - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday 27 January 2023

WAHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA KUIBA MAFUTA YA UJENZI WA SGR

Mahakama ya wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza imewahukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini washtakiwa watatu kati ya sita waliohusika na wizi wa mafuta ya petroli yaliyokuwa yanatumika katika ujenzi wa reli ya kisasa SGR.
Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi mwandamizi wa mahakama hiyo John Jagadi amesema washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka matatu yakiwemo ya kupatikana na mali ya wizi, kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni pamoja na kufanya biashara ya mafuta ya petroli katika mazingira hatarishi ambapo washtakiwa hao walikiri makosa mawili.


Katika kesi namba 15 inayomkabili Levy Daniel na Fredy Magay ambao walikamatwa mnamo tarehe 23 na mafuta ya petroli lita nne na wakakiri kosa moja kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni.


Katika shtaka la kufanya biashara bila kuwa na leseni hakimu Jagadi amesema kwa mujibu wa kifungu namba 132 kifungu kidogo cha kwanza na cha nne cha sheria ya udhibiti wa nishati washtakiwa hao watatakiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka miwili au kulipa faini ya shilingi laki moja kila mtu.


Aidha katika kesi nyingine namba 9 ya mwaka huu inayomkabili Dotto Ihanu ambae amekiri kufanya biashara ya mafuta bila kuwa na leseni pamoja na kuuza mafuta ya petroli katika mazingira hatarishi ambapo mnamo tarehe 23 ya mwaka huu wilayani Kwimba alikamatwa na lita 21 za mafuta ya petrol.


Katika shtaka la kufanya biashara bila kuwa na leseni mahakama hiyo imemhukumu kifungo cha miaka miwili gerezani au kulipa faini ya shilingi laki moja na elfu hamsini huku katika shtaka lingine la kufanya biashara ya mafuta katika mazingira hatarishi akihukumiwa kwenda gerezani miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki moja.


Mahakama imesema washtakiwa wote watatu kama wakifanikwa kulipa faini shtaka moja la kupatikana na mali ya wizi lina dhamana na wakikidhi masharti ya dhamana watakuwa huru huku kesi hiyo ikipangwa tena hadi tarehe 9 ya mwezi wa pili mwaka huu.


chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso