TIMU YA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WANAFUNZI KUFUNDISHWA KULAWITIANA YATUMWA KILIMANJARO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 17 January 2023

TIMU YA KUCHUNGUZA TUHUMA ZA WANAFUNZI KUFUNDISHWA KULAWITIANA YATUMWA KILIMANJARO

Wizara ya Elimu, Sayansi na Elimu ya Juu, imetuma timu maalumu mkoani Kilimanjaro kuchunguza tuhuma za wanafunzi kufundishwa vitendo vya ulawiti katika shule mkoani humo.


Uamuzi wa Serikali unatokana na gazeti moja nchini kuripoti uwepo wa shule inayofundisha masuala hayo mkoani humo kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Mtanzania.


Akizungumza leo Jumanne Januari 17, 2023 katika viwanja vya Bunge, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema timu hiyo inaongozwa na Kamishna wa Elimu nchini na inajumuisha mwanasheria wa wizara hiyo na mkurugenzi wa udhibiti ubora.


Amesema mbali na hatua hiyo, wamewasiliana na Mkuu wa Mkoa iwapo kuna jinai yoyote ili hatua za kisheria zichukuliwe mara moja katika kukomesha vitendo hivyo.


"Timu imeashaanza uchunguzi katika shule zilizotajwa na hatua za haraka zitachukuliwa kwa wahusika wote watakaobainika kuhusika na kadhia hiyo,” amesema Profesa Mkenda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso