MWILI WA KICHANGA WAOKOTWA NA RAIA WEMA KWENYE BOMBA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 10 January 2023

MWILI WA KICHANGA WAOKOTWA NA RAIA WEMA KWENYE BOMBA

Wakaazi wa eneo la Kawangware Nairobi nchini Kenya, wamebaini mwili wa mtoto mchanga uliotupwa kwenye bomba la maji taka. Mwili huo uligunduliwa na waendesha bodaboda waliokuwa wameegesha karibu na Shule ya Upili ya St.Anthony.
Sehemu ambayo mwili wa kichanga umeonekana


Kulingana na wakazi hao, mwili huo ulikuwa bado mbichi, ishara kwamba ulikuwa umezaliwa saa chache mapema, pengine Jumamosi usiku.


Kufuatia tukio hilo , Mwenyekiti wa eneo la Nyumba Kumi Joel Githinji, amepinga kitendo hicho kwa kukitaja kuwa cha kikatili na amewataka wanawake kukubali majukumu ya uzazi pindi wanapobaini ni wajawazito badala ya kutoa mimba zisizotarajiwa kwani zinaweza kuhatarisha maisha yao.


Pia amewashauri waepuke uhusiano na wanaume wasiowajibika na wapenda starehe za mwili tu kwani hawawezi kubeba majukumu ya wazazi.


chanzo:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso