KICHANGA CHA SIKU NNE CHATUPWA NA BABA MZAZI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 5 January 2023

KICHANGA CHA SIKU NNE CHATUPWA NA BABA MZAZI

Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Geita limefanikiwa kuokoa mwili wa kichanga cha siku nne kilichokuwa kimetupwa na baba mzazi wa kichanga hicho kwenye dampo la takataka majira ya saa tatu asubuhi ya Jana Januari 4/2023.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema baba wa kichanga hicho alifika na boksi likiwa na mwili na kulitupa kwenye dampo la takataka na kukimbia.


Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Geita Dokta Pascalates Mujuni anasema walimpokea mama wa kichanga hicho anayefahamika kwa jina la Emmanuelina Melikioli, Desemba 31, saa 10 jioni kama rufaa kutoka hospitali ya wilaya ya Nzera akiwa na tatizo la kupungukiwa Damu na mtoto kutocheza tumboni kwa siku tatu.


Ameeleza kuwa ilipofika saa 1 usiku mama huyo alijifungua kwa njia ya kawaida mtoto akiwa amefariki ma hadi sasa mama wa kichanga hicho bado anapatiwa matibabu.


Muda mchache baada ya baba wa mtoto kutupa mwili wa kichanga hicho jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kufika na kuuchukua mwili huo na kuurudisha hospitali kwa ajili ya taratibu za mazishi.


CHANZO: EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso