AKATISHA MASOMO BAADA YA KUBAINIKA KUWA NA MIMBA YA MIEZI 7 - SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday 12 January 2023

AKATISHA MASOMO BAADA YA KUBAINIKA KUWA NA MIMBA YA MIEZI 7 - SHINYANGA


Binti Mwenye miaka 13 mkazi wa Pandagichiza Halmashauri ya Shinyanga amekatisha masomo yake baada ya kupewa ujauzito akiwa darasa la sita katika mojawapo ya shule za msingi katika Kata hiyo ambapo kwa sasa ujauzito huo una umri wa miezi 7.



NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Tukio hilo limetokea mwishoni mwa mwaka 2022 katika kijiji cha Sayu Kata ya Pandagichiza halmashauri ya Shinyanga Mkoani humo.


Akieleza juu ya tukio hilo Baba mdogo wa mhanga,Emmanuel Nzenzule,Amesema jambo hilo alilikuta limetokea ambapo walienda katika shule aliyokuwa akisoma mtoto huyo na kuambiwa waende mjini kwaajili ya kupima afya ya binti ambapo walimkuta akiwa na miamba yenye miezi takriban 6 ndipo walipoenda shule ili kuzungumza na Mwalimu mkuu baba wa kijana aliyetenda tukio na walezi wa mhanga huyo.


“Walimpeleka mjini kumpima Mtoto wakamkuta yupo na mimba ya miezi 6 ikabidi waende shu;le kwaajili ya kuzungumza na mwalimu mkuu,baba wa kijana aliyetenda tukio hilo na walezi wa mhanga huyo ambapo mzazi wa kijana huyo alitozwa laki 6 na walezi wa binti na tukio kuishia hapo hapo”Amesema Nzenzule.


Kwa upande wake Mtendaji wa kijiji cha Sayu,Rwambo manzani,Amesema Majira ya saa 5 usiku alipewa taarifa za tukio hilo na mwalimu mkuu ambapo walikuwa tayari wameisha mpeleka binti huyo Hospitaliambapo alichukua hatua ya kuwatafuta Polisi jamii(Sungusungu) kwaajili ya kumtafuta aliyehusika na ubakaji huo.


Manzani,amesema awali alijua tukio hilo limeripotiwa polisi jambo ambalo siyo sahihi ndipo alipokuja kuambiwa na Afisa maendeleo kuwa kuna taratibu zinafanyika chinichini za kusuluhisha na kumaliza tatizo hilo pasina kufikisha malalamiko kwenye Jeshi la Polisi.


Aidha kwa upande wake Afisa Mtendaji Kijiji cha Pandagichiza,Theresia Shijja,Amesema tukio la binti kupewa mimba ni kweli lilitokea ambapo alipigiwa simu na mwalimu wakiwa wanatoka kumpima sambamba na kufanikiwa kuzungumza na binti huo na kuweza kumjua kijana aliyetenda tukio hilo ambapo alimtafuta na kufanikiwa kumkamata.


”Tukio la binti kweli lilitokea na baada ya kutokea nililetewa taarifa na mwalimu wakitoka kwenye vipimo,nilimuhoji binti akafanikiwa kunitajia jina la kijana aliyemfanyia hivyo,basi nikatumia mbinu za kumtafuta Yule kijana na kufanikiwa kumkamata kwaiyo nikawa nao wote nikawaambia sina mamlaka ya kutatua kesi kama hizi nikawa nimewaandikia barua ya kwenda polisi lakini kabla hawajaenda polisi alikuja mgambo na kusema wanahitajika kwa Mtendaji wa Kata”Amesema

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso