WANANCHI MKOA SHINYANGA WAASWA KUTOA TAARIFA ZA RUSHWA YA NGONO,RPC MAGOMI ASEMA WABADHILIFU WOTE WATACHUKULIWA HATUA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday 18 December 2022

WANANCHI MKOA SHINYANGA WAASWA KUTOA TAARIFA ZA RUSHWA YA NGONO,RPC MAGOMI ASEMA WABADHILIFU WOTE WATACHUKULIWA HATUA

Wananchi wa Mkoa wa Shinyanga wameaswa kupinga na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa ya ngono kwa wanawake ili kuwepo na haki na usawa sambamba na kutokomeza vitendo vya ukatili katika jamii.

Kamanda wa Polisi Mkoa Janeth Magomi akiwa anafungua rasmi semina ya kupinga na kukataa rushwa ya ngono Mkoa wa Shinyanga.


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Akizungumza katika Zoezi la Uzinduzi wa Kampeni ya Rushwa ya ngono,lililofanyika Desemba 17,Mwaka huu kwenye uwanja wa Kambarage,Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,amesema.


Rushwa ya ngono kwa wanawake imekithiri katika nyaja zote,Ofisini,mashuleni na katika mitandao ya kijamii ambapo kumekuwa na watu wanaofanya ukatili wa kijinsia kwa kuwaomba Rushwa ya ngono mabinti na wanawake ili kuwatimizia mahitajio yao hali inayopelekea kupata mimba zisizotarajiwa sambamba na kujipatia maradhi yasiyokuwa na tiba.


Mara baada ya kufungua Kampeni hiyo,RPC Janeth Magomi,amesema kuwa kampeni hiyo itakuwa ni endelevu ambapo Jeshi la polisi litashirikiana na wananchi kuwabainisha waovu wote wanatoa na kupokea rushwa ya aina yeyote.


Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga,John Tesha,Amesema maendeleo yanayopatikana katika manispaa hiyo hupatikana kukingana na kuwepo kwa wafanyajazi na watumishi waaminifu ambao hawatendi vitendo vya Rushwa ya aina yeyote(Fedha na ngono) hali inayo iweka salama Manispaa hiyo.


"Maendeleo haya hayawezi kuwa endelevu kukiwa na rushwa,tuendelee kushirikiana kutoa taarifa na kupinga vitendo vya rushwa ili kuweza kuijenga manispaa yetu kuwa imara"Amesema Tesha.


Nae Mkurugenzi wa Karibu Tanzania Organization(KTO),Maggid Mjengwa,Amewataka wananchi na wakazi wa Mkoa Shinyanga kufahamu ya kuwa rushwa ya ngono na rushwa zingine zinawahusu watu wote ambapo amesema kwa kushirikiana wananchi wote kuwabainisha na kuwachukulia hatua wanaojihusisha na rushwa ili kutokomoza janga hilo katika jamii.

Mkurugenzi wa Shirika la Karibu Tanzania Organization (KTO) Maggid Mjengwa akizungumza katika ufunguzi wa semina ya kukataa rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.

Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga Ndugu John Tesha  akitoa neno katika ufunguzi wa semina ya kukataa rushwa ya ngono Mkoani Shinyanga.

Afisa wa TAKUKURU Mkoa Shinyanga,Rauben Chongolo,Akiendelea na semina ya uelewa juu ya rushwa ya ngono kwa waandishi wa habari na waendesha baiskeli mkoani Shinyanga. 


Mkuu wa chuo cha Maendeleo ya wananchi Buhangija(FDCs),Maria Mkanwa,akizungumza wakati wa kutoa semina kwa waandishi wa habari na waendesha baiskeli mkoani Shinyanga. 


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso