RTO SHINYANGA DEBORA LUKOLOLO AONYA BODABODA WANOPAKIA NONDO NA MBAO NDEFU BILA VIOO ANGALIZI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday 13 December 2022

RTO SHINYANGA DEBORA LUKOLOLO AONYA BODABODA WANOPAKIA NONDO NA MBAO NDEFU BILA VIOO ANGALIZI.

Baadhi ya wananchi Mkoa Shinyanga wamewalalamikia waendesha pikipiki maarufu kama boda boda wanaosafirisha vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na mbao ndefu,mabati,Nondo na square pipe hali inayohatarisha usalama wa raia pamoja na watumiaji wote wa barabara.

Afisa Usalama barabarani (RTO) Debora Lukololo akizungumza na wendesha boda boda.


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.


Wakizungumza na waandishi wa habari wananchi hao wamesema bodaboda hao wamekua wakibeba mizigo bila kuweka viakisi mwanga jambo ambalo limekua likihatarisha maisha yao sambamba na ya watumiaji wa barabara.


Aidha wananchi hao wamebainisha kuwepo kwa ajali ambazo zimekua zikisababishwa na usafirishaji wa bidhaa hizo kama(mbao,mabati,nondo na square pipe),huku wakiiomba mamlaka husika kutoa adhabu kali kwa madereva wa bodaboda wanaokiuka sheria za barabarani.


Akizingumza kwa niaba ya bodaboda,Fred Felix,amesema kuwa lengo la kuendesha bodaboda ni kujitafutia rizki huku akibainisha kuwepo kwa madereva wa pikipiki wanaokiuka sheria walizowekea na Traffic kwa kupakia mbao hali inayohatarisha usalama wa watu na mali zilizopo pembezoni mwa barabara.


Kwa upande wake Katibu wa soko la Mbao Chamaguha,Abdallah Ahmad,amesema kuwa sheria za barabarani zimeshafundishwa kwa watumiaji wa vyombo vya moto lakini bado kumekuwa na uwepo wa bodaboda wanaokiuka sheria kwa kubeba bidhaa hizo ambapo hawakamatwi na traffic.


“Ni kweli kumekuwa na bodaboda wanaobeba mbao licha ya elimu ya usalama barabarani ambayo ilitolewa lakini bado sheria hazifuatwi wala hakuna hatua yeyote inayochukuliwa kwa bodaboda wanaokwenda kinyume,tunaomba mamlaka husika iliangalie hili”Amesema Ahmad.


Aidha kwa Kwa upande wake Afisa Usalama barabarani,RTO, Debora Lukololo,amesema kuwa kumekuwa na waendesha pikipiki wanaopakia bidhaa ambazo zinahatarisha usalama kwake na watumiaji wengine wa barabara sambamba na kutokuwepo na vioo angalizi(Site mirror)kwenye pikipiki zao,ambapo amesema hataki kuona aina hiyo ya usafirishaji na kuwataka wawaachie madereva wa magari kupakia bidhaa hizo ili kuepusha ajali.


“Ajali nyingi sasa ivi ni za bodaboda,mnapakia abiria wengi(Mishikaki),mnaendesha mwendo mbaya,hamtii taa za barabarani ,mnabeba bidhaa ndefu kiasi kwamba mnafunga barabara,nikikukamata pikipiki yako itaozea kituoni,niwatake mkawe watiifu kwenye usafirishaji wenu wa abiria”Amesema Debora.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso