VIBAKA WAVAMIA MOCHWARI NA KUONDOKA NA MWILI. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday 10 December 2022

VIBAKA WAVAMIA MOCHWARI NA KUONDOKA NA MWILI.

Mhudumu wa mochwari katika Kaunti ya Nayandarua nchini Kenya alibaki kinywa wazi, mapema Alhamisi asubuhi baada ya watu wasiojulikana kuvunja makafani hiyo na kuiba mwili.



Joseph Mbuthia Githundi, ambaye anafanya kazi kwenye mochari ya Hospitali ya JM, alipigwa na butwaa baada ya kupata kwamba watu wasiojulikana walivamia mahali hapo usiku wa Jumatano.


Kwa mujibu wa ripoti ya Nation.Africa, maiti iliyotoweka kwenye friji ilikuwa ya mvulana wa miaka 10, na polisi hatimaye waleweza kuipata kwenye 'septic tank' iliyoko karibu na mochari hiyo baada ya kuitafuta.


Mwili huo ulipatikana salama na kurejeshwa kwenye mochari, huku uchunguzi wa tukio hilo ukianza.


Ripoti zimebaini kwamba wafanyakazi wa vibarua waliokuwa wakiandamana kupinga kufutwa kazi na serikali ya kaunti huenda walihusika na tukio hilo, ila polisi wameahidi kufanya uchunguzi wa kina.


Kwa upande wake, Naibu kiongozi wa wengi wa Bunge la Nyandarua Mwangi Kagwe, alisema kuwa hospitali hiyo haitachukua miili yopyote hadi pale usalama utakapoimarishwa.


“Tumefanya mazungumzi na maafisa wa idara ya afya na tumekubaliana kwa mambo kadhaa ikiwemo, usalama kuimarishwa na ukuta kujengwa kwenye mochari hiyo,” MCA huyo aliongeza kusema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso